Abbas aanza ziara ya siku tatu nchini Lebanon
21 Mei 2025Rais wa mamlaka ya ndani ya Wapalestina Mahmud Abbas anaanza ziara ya siku tatu nchini Lebanon. Mwanachama wa kamati kuu ya chama cha ukombozi wa Wapalestina PLO,
Ahmad Majdalani, ambaye ameandamana na Abbas katika ziara hiyo amesema suala la silaha katika kambi ya wakimbizi wa Kipalestina nchini Lebanon litakuwa katika ajenda ya mazungumzo kati ya rais Abbas na rais wa Lebanon Joseph Aoun pamoja na serikali ya nchi hiyo.
Rais Mahmoud Abbas awataka Hamas waachie mamlaka ya Ukanda wa Gaza
Ziara ya Abbas inafanyika baada ya rais wa Lebanon kusema mwishoni mwa mwezi uliopita kwamba mamlaka walikuwa wakifanya kazi ya kuondosha silaha zote nzito na za wastani ambazo hazijaidhinishwa kutoka maeneo yote ya Lebanon na kwamba atalijadili suala la kuondosha silaha katika kambi za wakimbizi wa Palestina na rais Abbas.