Juhudi za uokoaji zaendelea Myanmar na Thailand baada ya tetemeko kubwa la ardhi. Maelfu ya waandamanaji waingia barabarani katika mitaa ya Istanbul, Uturuki kudai kuachiwa huru kwa kiongozi mkuu wa upinzani Ekrem Imamoglu. Wizara ya afya huko Gaza imesema watu zaidi ya 900 wameuawa tangu Israel ianzishe wimbi jipya la mashambulizi.