Rais wa Marekani Donald Trump awatolea wito Putin na Zelensky kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano. Watu wanane wauawa nchini Yemen kufuatia mashambulizi ya Marekani dhidi ya waasi wa Kihouthi. Na ripoti ya SIPRI imesema matumizi ya kijeshi duniani kote yameongezeka mwaka jana na kwa kasi zaidi tangu kumalizika kwa Vita Baridi.