Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Makubaliano ya amani yanatarajiwa kutiwa saini leo Ijumaa huko Washington kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda / Shirika la Kutetea Haki za Binaadamu la Human Rights Watch limesema mamlaka nchini Kenya zinapaswa kuwajibikia dhuluma zote zilizofanywa wakati wa maandamano ya nchi nzima ya tarehe 25 Juni, 2025