Matangazo
Miongoni mwa yaliyomo kwenye habari za ulimwengu:
Wajerumani katika jimbo dogo la magharibi la Saarland leo wanapiga kura katika uchaguzi unaotizamwa kama kipimo kinachobaini ushawishi wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel dhidi ya washindani wake.
Mgombea urais nchini Ufaransa Emmanuel Macron apata uungwaji mkono zaidi baada ya maseneta 9 wa siasa za mrengo wa wastani-kulia kuamua kumuunga mkono.
Raia wa Bulgaria wafanya uchaguzi kwa mara ya tatu ndani ya miaka minne, uchaguzi unaoweza kuisogeza nchi hiyo karibu na Urusi kuliko Umoja wa Ulaya.