Wajumbe wa Urusi na kutoka Ukraine wanakutana mjini Istanbul kwa mazungumzo// Burundi imefanya uchaguzi wa maseneta leo Jumatano kujaza nafasi za chombo hicho cha maamuzi kinachowakilisha mikoa 5 ya nchi hiyo// Mfumo wa elimu nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo umetumbukia kwenye msukosuko baada ya mwaka wa masomo kufikia mwisho mwezi Juni bila ya wanafunzi kupatiwa nakala rasmi za matokeo yao.