Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Kifo cha Mohamed Abdulrahman, ambaye kabla ya kustaafu kwake mwaka 2019 alikuwa mhariri na naibu msaidizi wa mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW / Wajumbe wa Bunge la Ulaya wameutaka Umoja wa Ulaya kusitisha misaada ya kifedha kwa nchi za Afrika zinazowaminya wapinzani na kuwazuia kushiriki chaguzi za kisiasa