11 wafungwa Georgia kwa kuandamana
3 Septemba 2025Haya ni kwa mujibu wa shirika moja la habari nchini humo.
Shirika la habari la Interpress nchini humo limeripoti kuwa mahakama moja mjini Tbilisi imewakuta na hatia waandamanaji 11 akiwemo muigizaji maarufu nchini humo Andro Chichinadze.
Mahakama hiyo imedai kuwa waandamanaji hao walitatiza amani ya umma wakati wa maandamano ya kuipinga serikali mwaka uliopita.
Waandamanaji wengine 8 wafungwa jela
Hiki ni mojawapo ya visa ambavyo wakosoaji wanaviona kama visa vya kuwakandamiza wakosoaji nchini humo.
Hukumu hiyo inakuja siku moja baada ya mahakama kuwafunga jela kwa kati ya miaka 2 na miaka miwili na nusu waandamanaji wengine 8 kwa mashtaka kama hayo.
Georgia ambayo ni nchi rasmi inayotarajiwa kujiunga na Umoja wa Ulaya, imekuw aikikabiliwa na miezi kadhaa ya machafuko ya kisiasa tangu uchaguzi wa bunge uliopingwa na upinzani mwezi Oktoba, ambapo chama tawala Georgian Dream Party kilitangaza ushindi.
Vyama vya upinzani vinakituhumu chama hicho tawala kwa wizi wa kura, kuelekea njia ya utawala wa kidikteta na kujisogeza karibu na Moscow- - madai yanayopingwa na chama hicho.