Chama cha upinzani nchini Tanzania, ACT-Wazalendo leo kimefanya mkutano wake mkuu na kuwachagua aliyekuwa mbunge wa CCM, Luhaga Mpina na kada wa ACT Aaron Kalikawe, kuwa wagombea wa urais kupitia chama hicho// Rais wa Burundi, Évariste Ndayishimiye amewaapisha mawaziri 13 wa serikali mpya inayoongozwa na Waziri Mkuu Nestor Ntahontuye baada ya kufanya mabadiliko makubwa hapo jana//