Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Mpango wa Israel wa kutanua operesheni zake huko Gaza na kutangaza nia ya kuliteka eneo lote la ukanda huo na kusalia katika ardhi hiyo ya Palestina kwa muda usiojulikana umepingwa na mataifa mbalimbali / Vyama vya CDU/CSU nchini Ujerumani, vimetia saini makubaliano ya kuunda serikali ya pamoja yanayofungua njia kwa utawala mpya.