Wakati rais wa Marekani Donald Trump akisema kuwa mpango wa usitishwaji mapigano kwa siku 60 huko Gaza unakaribia kufikiwa, kundi la Hamas limeeleza kuwa bado mazungumzo yanaendelea// Wakati mapambano kati ya waasi wa M23 na majeshi ya serikali ya Kongo yakiendelea mashariki mwa nchi hiyo, wanawake na wasichana wameendelea kuwa wahanga wakuu wa ukatili wa kingono.