Mawakili William Ruto wamelirai jopo la majaji 7 wa mahakama ya juu kuepusha mgogoro wa katiba kwani hakuna ushahidi kuwa uchaguzi mkuu wa Agosti ulikuwa na hila.Wakati huohuo,shughuli ya kuhesabu kura upya kutokea vituo 15 imekamilika. Kwa upande mwengine,kampuni ya teknolojia ya uchaguzi ya Smartmatic imekataa kutii amri ya mahakama ya kuzingua seva zake kwani ni ukiukaji wa haki ya uvumbuzi.